FRANKFURT:Marubani wa Lufthansa wagoma kwa saa mbili | Habari za Ulimwengu | DW | 31.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FRANKFURT:Marubani wa Lufthansa wagoma kwa saa mbili

Kampuni ya Ndege ya Ujerumani Lufthansa imefuta safari 18 za ndege zinazoendeshwa na kitengo chake cha City Line baada ya marubani kugoma kwa saa mbili asubuhi ya leo.Mgomo huo ulianza saa kumi na mbili u nusu hadi saa mbili u nusu na kuathiri safari zinazoanzia hapa Ujerumani.

Kitengo cha City Line hutoa huduma za safari za ndege hapa nchini hadi miji 60 barani Ulya na kusafirisha takriban abiria milioni 6.7 kwa mwaka.Shirika la Marubani lilifanya mgomo huo baada ya mazungumzo kati yao na Kmapuni ya Lufthansa kukwama,Majadiliano hayo yalilenga kusawazisha utendaji kazi kwa jumla likiwemo suala la saa nyingi za kazi na siku chache za mapumziko kwa marubani.Ndege zilianza safari zake tena baada ya saa mbili unusu asubuhi japo idadi kamili ya abiria walioathirika haijulikani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com