Finali ya kombe la Ulaya | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 27.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Finali ya kombe la Ulaya

Nani atatoroka na kombe jumapili ? Ujerumani au Spain ?

German Chancellor Angela Merkel (L) and Bastian Schweinsteiger

German Chancellor Angela Merkel (L) and Bastian Schweinsteiger

Spain jana iliikomea Urusi mabao 3:0 na kupanga miadi na Ujerumani kwa finali ya kombe la Ulaya 2008 katika uwanja wa Eranst Happel kesho kutwa jumapili.

Ujerumani maadui zao, watolewa jasho na Uturuki kabla ya dakika ya mwisho ya 90 Philipp Lahm,mlinzi wao kuwapatia bao la ushindi.Rais Horst Kohler wa Ujerumani na hata Kanzela Angela Merkel, wameshatangaza kuhudhuria finali hiyo mjini Vienna.

►◄

Kanzela Angela Merkel,amekuwa shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Ujerumani na alikuwa uwanjani i ilipoitimua Uturuki kwa mabao 3-2 na kukata tiketi yake ya finali na Spain.Atahudhuria finali ya jumapili.Yamkinika akafuatana na mawaziri wake kadhaa mjini Vienna,kuiona Ujerumani ikitwaa kombe la ulaya kwa mara ya 4 baada ya 1996 uwanjani Wembley,London.

Bao la ushindi la Lahm, lilishusha pumzi za wajerumani wote pamoja na kanzela wao Kanzela Angela Merkel,aliekua uwanjani:

"Nikishindwa kushusha pumzi-naipongeza timu yetu,lakini lazima pia, niwape heko waturuki.Tumeshinda na tunafurahia ushindi wetu."

Alisema Kanzela wa Ujerumani shabiki wa dimba.

Waspain nao walishangiria ushindi wao wa mabao 3:0 dhidi ya Urusi jana na sasa wanaamini watarudi Madrid na kombe jumapili hii na hivyo kukata kiu kirefu.Spain ilicheza finali mara ya mwisho miaka 24 iliopita 1984 na kulazwa na Ufaransa.

Wakishinda jumapili,itakua tena fiesta katika mitaa ya Madrid na Barcelona kama ilivyokua jana baada ya firimbi ya mwisho kulia walipoitoa Urusi:

Shabiki mmoja wa Spaina alisema:

"Ujerumani daima inafika mbali,hatahivyo sikitu,Spain ni imara na itatamba pamoja na chipukizi weo Torres."

Spain imeingia mara mbili finali ya kombe la Ulaya hapo kabla.Ilitawazwa mabingwa 1964 na kutawazwa bingwa.Katika finali ya pili ilitoka mikono mitupu ilipocheza na Ufaransa, 1984. Jumapili hii basi, inataka kukata kiu cha miaka 44 tangu ilipotwaa kombe.

Ujerumani,ni mabingwa mara 3 wa ulaya na dunia na walilitwaa kombe hili mara ya mwisho,1996 uwanjani wembley,uingereza walipoilaza Jamhuri ya Czech kwa bao kitanzi la meneja wao wa sasa Oliver Bierhof.

Ujerumani nzima inaamini,licha ya misukosuko iliopata Ujerumani ilipocheza na Croatia na hata Uturuki, Ujerumani ina ari na uvumilivu wa kumudu zahama na vishindo hadi firimbi ya mwisho.Ukiwa huamini hayo, waulize waturuki walikiona nini dakika ya 90 hivi majuzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com