1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dushanbe.Rais Emomali akataa vigezo vya nchi za Magharibi katika uchaguzi wa Tajikistan.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvT

Rais wa Tajikistan, Emomali Rakhmonov amesema, uchaguzi wa Urais unaofanyika nchini mwake, hautafanyika kwa vigezo vya nchi za Magharibi.

Baada ya kupiga kura yake hii leo Rais, Emomali amesema, Tajikistan ina „utamaduni tofauti“ na hivyo hakuna haja kwa nchi za Asia kujiambatanisha na „maadili mapya“.

Rais Emomali Rakhmonov anaegombea Urais kwa kipindi kingine cha miaka saba, anatazamiwa kushinda katika uchaguzi ambao umesusiwa na vyama vikuu vya upinzani.