Tembelea tovuti mpya ya DW

Tazama toleo la beta la dw.com. Bado hatujamaliza! Maoni yako yanaweza kutusaidia kuiboresha.

  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Francois Fillon

Francois Fillon ni mwanasiasa wa Ufaransa na alieshikilia wadhifa wa waziri mkuu chini ya utawala wa Nicolas Sarkozy kati ya 2007 hadi 2012. Ndiye mteule wa sasa wa chama cha Republican kuwania nafasi ya rais.

Kupitia jukwaa linaloelezwa kuwa la wahafidhina, Fillon alijitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican. Alionekana kama chaguo la tatu hata wiki moja kabla ya kura ya kwanza iliyofanyika Novemba 20. Hatimaye alishika nafasi ya kwanza na kumshinda Alain Juppe katika duru ya pili ya uchaguzi wa mchujo wiki mbili baadae. Kufuatia ushindi wake, uchunguzi wa maoni ulimuonyesha kama mmoja wa wagombea wa usoni sambamba na Marine Le Pen wa siasa kali za mrengo wa kulia na Emmanuel Macron wa mrengo wa wastani. Fillon amejikuta katika kashfa baada ya kuibuliwa taarifa kwamba alikuwa akimlipa mke wake mshahara wa serikali pasipo kufanya kazi yoyote. Alikataa kujitoa katika kinyanganyiro licha ya kutupwa mkono na wasaidizi wake wa karibu.

Onesha makala zaidi