DRESDEN : Umoja wa Ulaya wakutana kujadili wahamiaji | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DRESDEN : Umoja wa Ulaya wakutana kujadili wahamiaji

Nembo ya Shirika la haki za binaadamu-Amnesty International, lililotoa ripoti hiyo.

Nembo ya Shirika la haki za binaadamu-Amnesty International, lililotoa ripoti hiyo.

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya wa sheria na mambo ya ndani wameanza mazungumzo ya siku tatu yenye kulenga kimsingi njia za kuzuwiya kumiminika kwa wahamiaji wasio halali barani Ulaya.

Mazungumzo hayo yasio rasmi katika mji wa mashariki ya Ujerumani wa Dresden ni ya kwanza kufanyika tokea kutanuka kwa Umoja wa Ulaya hadi kuwa na mataifa wanachama 27 kufuatia kujiunga kwa Romania na Bulgaria hapo tarehe Mosi Januari.

Kwa mara ya kwanza mawaziri hao wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa pia kuangalia njia za kufunguwa milango ya wahamiaji halali ili kusaidia kupambana na uhaba wa wafanyakazi barani Ulaya.

Ujerumani hivi sasa inashikilia Urais wa Umoja wa Ulaya wa ambao ni wa kupokezana kila baada ya miezi sita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com