Deutsche Bahn yapendekeza mpango mpya wa mishahara | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Deutsche Bahn yapendekeza mpango mpya wa mishahara

Shirika la reli la taifa nchini Ujerumani Deutsche Bahn limesema kwamba shirika hilo pamoja na vyama viwili vya wafanyakazi wa reli wamerasimu mfumo mpya wa mishahara kwa kwa matarajio kwamba utakubaliwa na chama cha tatu cha madereva wa treni GDL ambacho migomo yao hivi karibuni ilitibuwa usafiri wa treni za mizigo na abiria nchini.

Chama cha GDL chenye kuwakilisha madereva wa treni kimekuwa kikishinikiza makubaliano tafauti ya mishahara na Deutsche Bahn.Shirika hilo la reli la taifa linasema mfumo huo uliopendekezwa utapelekea ongezeko la mshahara la hadi asilimia 10 na malipo maalum kwa wafanyakazi binafsi wenye ujuzi wa kazi kwa wafanyakazi 150,000 wa shirika hilo.

Ongezeko hilo la asilimia 10 litajumuisha ongezeko la asilimia 4.5 lililokubaliwa mwezi wa Julai uliopita kati ya shirika hilo na vyama viwili vya wafanyakazi wa reli Transnet na GDBA.