Confederations Cup kufungua pazia la Kombe la dunia 2010 | Michezo | DW | 12.06.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Confederations Cup kufungua pazia la Kombe la dunia 2010

Firimbi italia kesho Johannesberg kuziita Iraq na Bafana Bafana.

default

Steven Pienaar (Bafana-Bafana na dimba)

Mabingwa wa Asia "simba wa Mesopotemia-Iraq", wana miadi kesho (jumapili) mjini Johannesberg, kufungua dimba la kombe la mashirikisho -Confederations Cup- na wenyeji wa Kombe lijalo la dunia Bafana Bafana -Afrika Kusini.Jumatatu siku ya pili yake,itakua zamu ya mabingwa wa Afrika "Mafirauni-Misri" kupimana nguvu na mabingwa wa Kombe hilo na wa Amerika kusini-Brazil.Klabu ya Al Merrreikh ya Sudan,imetangaza kufadhi maandalio ya kombe lijalo la klabu bingwa la CECAFA.Michel Platini,Rais wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya, astushwa na kitita cha rekodi ilichotoa Real Madrid ya Spain kumnunua Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United.Kesho (Jumapili) duru ya kwanza inaanza kunyanganyia kitita cha dala milioni 1 katika mashindano ya riadha ya Golden League:

Mwaka kabla firimbi kulia kuanzisha Kombe la Dunia la FIFA nchini Afrika Kusini na la kwanza barani humo katika historia ya Kombe hili,firimbi inalia kesho mjini Johannesberg,kufungua Kombe la mashirikisho-Confederations Cup linalojumuisha timu 8 zitakazogawiwa katika makundi 2 :(A na B) :

Kundi A linajumuisha wenyeji Bafana Bafana au Afrika Kusini wanaofungua dimba na mabingwa wa Asia-Iraq.Tena kuna mabingwa wa ulaya Spain na New Zealand.Kundi B ndilo kali zaidi na kunakotazamiwa mabingwa kuibuka: Kuna mabingwa wa kombe hili Brazil,mabingwa wa Afrika misri,mabingwa wa Dunia -Itali na Marekani. Mastadi kama vile Kaka na Robinho wat akuwa uwanjani.

Nje ya Kombe la mashirikisho, taarifa iliousangaza ulimwengu wa dimba kati ya wiki hii ilitoka Manchester United, mabingwa wa Uingereza:Baada ya kubisha muda mrefu ,mwisho maneno mazuri yalimtoa nyoka pangoni:Kwa kitita cha rekodi cha dala milioni 131, Manu ilisalim amri na kuipigia magoti Real Madrid kumuuza jogoo lake Cristiano Ronaldo. Kima hicho cha Euro milioni 94 kinapindukia kile alichouzwa stadi wa brazil kaka majuzi kutoka AC milan kuhamia pia Real Madrid.Mashabiki wengi wa Manu wakiambiwa wasitie wasi wasi hakuna mapatano ya kumuuza Ronaldo.

Kitita kikubwa kama hicho, kinawaumiza vichwa wengi.Rais wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya, mfaransa Michel Platini alistushwa na kiwango kikubwa kama hicho na hasa kimekuja muda mfupi baada ya kile cha mbrazil Kaka.Platini alisema, " vitita vikubwa kama hivyo vinatoa changamoto kwa maadi.li ya "fair play" ya moyo mwema wa kispoti.

Platini binafsi aliiachamkono St.Etienne klabu yake ya Ufaransa 1982 kujiunga na Juventus ya Itali.Akaja kuibuka "mchezaji-bora wa dimba wa mwaka wa ulaya,1983,1984 na tena 1985.Amesema UEFA shirikisho lake la dimba la Ulaya linapanga sasa kuchukua hatua kuzuwia malipo makubwa kama haya ya Cristiano Ronaldo wa Ureno.

Katika kinyanganyiro cha mwezi huu cha Kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika mashariki na kati-Kombe la CECAFA,AL MERREIKH ya Sudan ilitangaza ushirikiano katika kuandaa kinyanganyiro cha mwezi huu cha kombe hilo na kuisaidia Al Merreikh kujiandaa kwa Ligi ya klabu bingwa za afrika mwezi ujao.

Mabingwa hao wa Sudan ambao watashiriki katika Ligi ya timu 12 kabla kuonana na mahasimu wao wa nyumban i Al-Hilal katika Ligi ya Afrika hapo Julai 18, imejitolea kugharimia gharama zote za usafiri na makaazi za timu zote pamoja na viongozi wao.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu yoyote kujitolea kufadhili mashindano ya kimkoa.Al Merreikh kwa njia hii inataka kukuza usuhuba mwema wa timu za mkoa.Timu hii yenye maskani yake mjini Omduraman wana miadi na Atraco ya Ruanda,mathare united ya Kenya na Djibsat ya Djibouti katika kundi A la kinyanganyiro hicho.Kinyanganyiro cha kombe hili la klabu bingwa la CECAFA kitaanza Juni 30 hadi Julai 12.

RIADHA:

Bingwa wa masafa marefu wa Olimpik na dunia wa ethiopia Kenenisa Bekele na msichana wa Urusi anaeruka kwa upongoo(Pole vaulte) Yelena Isinbayeva ni wa kwanza kufikiriwa kutoroka na kitita cha dala milioni 1 unapoanza msimu wa Golden League.Mwishoe, lakini huenda mambo yakamalizika vyengine kama ilivyotokea ghafula mwaka uliopita: Golden League, ni mashindano ya miji 6 yanayoanza kesho katika Uwanja wa olimpik wa Berlin -kituo hapo Augusti cha mashindano ya riadha ulimwenguni:

Mashindano ya riadha ya Berlin maarufu kwa jina la ISTAF ni ya kwanza katika mlolongo wa yale ya "Golden League" yanayojumisha miji 6 kabla kitita cha "jackpot" cha dala milioni 1 kugawanywa.Endapo mwanariadha akishinda mashindano yake katika miji yote 6, hugawana kitita hicho au ikiwa ni mmoja hunyakua chote.

Ni wanariadha 3 tu waliofaulu kutoroka na kitita chote na 2 kati yao ni kutoka afrika na wote ni wanawake: Kwanza alikuwa mwanamsumbiji Maria Mutola,bingwa wa olimpik 2000 huko sydney katika mbio za mita 800.yeye alinya

Muandishi: Ramadhan Ali /AFPE/DPAE/

Mhariri: M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com