China imesaini makubaliano ya kufufua mradi wa TAZARA
21 Novemba 2025
Barabara hiyo ya reli iliyofadhiliwa na China miaka ya 70 kurahisisha usafirishaji wa shaba na uingizaji wa mafuta kupitia Tanzania, inabakia kuwa barabara muhimu ya kibishara na inaonekana kutoa ushindani katika mpango wa Marekani na Ulaya wa Ukanda wa Lobito, ambayo ni njia ya reli inayounganisha Angola, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mpango huo ulisainiwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa China Li Qiang nchini Zambia, ambayo ilikuwa ziara ya kwanza ya mjumbe wa taifa hilo kwa zambia ndani ya miaka 28. Rais Hakainde Hichilema aliusifu uwekezaji huo.
China ni miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara barani Afrika na imedhamiria kutumia rasilimali asilia za bara hilo ikiwemo shaba, dhahabu, lithiamu na madini adimu ya ardhini.