1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARDIFF: Uvutaji wa sigara wapigwa marufuku

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD8

Uvutaji wa sigara ndani ya majengo umepigwa marufuku nchini Wales kuanzia leo. Yeyote atakayepatikana akiwasha sigara ndani ya baa, mgahawa, ofisi na vyombo vya usafiri wa umma, atatozwa faini ya euro 74.

Sheria hiyo inatekelezwa pia nchini Scotland huku Ireland Kaskazini ikijiandaa kuanza kuitumia ifikapo tarehe 30 mwezi huu.

Uingereza nayo itaanza kuitumia sheria hiyo kuanzia tarehe moja mwezi Jalai mwaka huu.