CAPE TOWN:Maafisa wa magereza wakataa kukata rasta zao
3 Agosti 2007Matangazo
Maafisa watano wa magereza nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi kwa kukataa kukata rasta zao ndefu.Maafisa hao watano wanaofanya kazi katika jela ya Pollsmoor iliyoko nje ya mji wa Cape Town waliadhibiw akwa kukiuka sheria za mavazi ya katika huduma za magereza.
Watu hao watano wanapigwa marufuku kufika mahala pa kazi ila wanaendelea kupokea mishahara yao kamili wakisubiri matokeo ya rufaa.Kulingana na idara hiyo maafisa hao walipuuza onyo zilizotolewa za kukata nywele hizo ndefu.