Bush asema kunahitajika ushupavu kufikiwa makubaliano katika mkutano wa Annapolis
27 Novemba 2007Matangazo
ANNAPOLIS.Rais George wa Marekani ameonya kuwa kutahitajika kufikiwa kwa makubaliano magumu ili kufikiwa kwa mpango wa amani kati ya Israel na Palestina.
Rais Bush alisema hayo katika chakula cha jioni alichowaandalia wajumbe wanaoshiriki katika mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati yanayofanyika huko Maryland.
Nchi kadhaa za kiarabu zikiwemo Syria na Saudi Arabia zinaudhuria mkutano huo mkubwa unaofadhiliwa na Marekani. Syria na Saudi Arabia haziitambui Israel na kushiriki kwao wachambuzi wa mambo wanasema kunaonesha ugumu wa mafanikio.