BRUSSELS: Viongozi wa Umoja wa Ulaya wajaribu kuafikiana | Habari za Ulimwengu | DW | 22.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Viongozi wa Umoja wa Ulaya wajaribu kuafikiana

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamerejea kujadiliana katika mkutano wao wa kilele,mji mkuu wa Ubeligiji, Brussels.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais unaozunguka katika Umoja wa Ulaya,amesema,yeye na viongozi wenzake, wanajitahidi kupata makubaliano kuhusika na mswada wa mageuzi ya mkataba wa umoja huo ulio na wanachama 27.Hata mkuu wa masuala ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,ana matumaini mema.

Kwa mujibu wa Kansela Merkel,mkataba huo utarahisisha utaratibu wa kupitisha maamuzi katika Umoja wa Ulaya unaopanuka.Lakini Uingereza,Jamhuri ya Czech,Uholanzi na Poland zinapinga baadhi ya mageuzi.

Mkataba huo utachukua nafasi ya katiba iliyoshindwa kupitishwa baada ya wapiga kura nchini Uholanzi na Ufaransa kuikataa katika kura ya maoni miaka miwili iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com