1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya yaishinikiza Sudan

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCj5

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameitaka serikali ya Sudan kuidhinisha kwa haraka uwekaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa katika jimbo la Dafur lililoathiriwa na vita.

Wakikutana mjini Brussels Ubelgiji mataifa ya Umoja wa Ulaya yametowa taarifa ya pamoja yenye kusema kwamba zina wasi wasi na kuendelea kwa umwagaji damu huko Dafur.

Serikali ya Sudan imekataa uwekaji wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa kadhalika lile la mchanganyiko wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Ujerumani ambayo inashika wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya kuanzia Januari Mosi mwakani imesema itajitahidi kufanikisha lengo la kuwa na katiba ya Umoja wa Ulaya.