Brown apanga upya baraza lake la mawaziri | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Brown apanga upya baraza lake la mawaziri

Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ameitumia siku yake ya kwanza madarakani,kuteua baraza lake jipya la mawaziri.

David Miliband akienda kupokea wadhifa wake mpya kama waziri wa nje wa Uingereza

David Miliband akienda kupokea wadhifa wake mpya kama waziri wa nje wa Uingereza

Baraza hilo la mawaziri ladhihirisha mtengano mkubwa na serikali ya waziri mkuu wa zamani Tony Blair.Waziri wa ulinzi Des Browne ni waziri pekee aliebakia na wadhifa aliokuwa nao katika serikali ya Blair.Mawaziri wapya saba wameteuliwa kwa mara ya kwanza,wakati 10 wengine ama wamefukuzwa,wameshushwa vyeo au wamejiuzulu.Alistair Darling,amechukua nafasi ya Gordon Brown kama waziri wa fedha na David Miliband ni waziri mpya wa masuala ya nje.Akiwa na umri wa miaka 41,Miliband ni waziri kijana kabisa kushika wadhifa huo tangu miongo mitatu.Na Jacqui Smith ni mwanamke wa kwanza nchini Uingereza,kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com