BRASILIA:Rais wa Brazil amfukuza kazi waziri wake wa ulinzi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRASILIA:Rais wa Brazil amfukuza kazi waziri wake wa ulinzi

Rais Luiz Inacio Lula da Silva amemfukuza kazi waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, kufuatia ajali ya ndege wiki iliyopita.Wizara ya Ulinzi ya Brazil ndiyo inayohusika na usalama wa anga.

Waziri huyo aliyefukuzwa kazi Waldir Pires amekuwa akikabiliwa na shutma kutokana na mtafuruku uliyoikabili sekta ya usafiri wa anga kwa kipindi cha karibu mwaka mmoja sasa.

Wiki iliyopita ndege ya shirika la ndege ya TAM iligonga jengo mmoja kwenye uwanja wa ndege wa Congonas ambapo watu zaidi ya mia mbili waliuawa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com