BONN: Mkutano wa mataifa ya ACP wafanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 13.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BONN: Mkutano wa mataifa ya ACP wafanyika

Mkutano wa mawaziri wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya watakutana leo huko Petersburg kitongoji cha Bonn na wenzao kutoka mataifa ya Afrika, eneo la bahari ya Pacific na Karibean kuzungumzia juu ya mkataba wa kibiashara.

Mkataba huo unatakiwa kusainiwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri wa biashara wa Nigeria, Jacob Gyeke Buba, amesema imechukua muda mrefu kwa Umoja wa Ulaya kufikia ulipo hivi sasa.

Aidha amesema viongozi wa umoja huo wamefaulu kwa kuyaweka pamoja maswala mengi na kuyashuhgulikia na akasema lazima kuwe na wakati ambapo Umoja wa Afrika utaweza kuyaweka mambo pamoja na kuzungumza kwa kauli moja kama Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com