BISHKEK: Uhasama wa kisiasa wazusha machafuko katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BISHKEK: Uhasama wa kisiasa wazusha machafuko katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek

Kumetokea machafuko katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek kati ya watu wanaoipendelea serikali na waandamanaji wafuasi wa upinzani. Polisi wameingilia kati na kutumia gesi za kutoa machozi kuwatawanya watu hao. Ghasia zimezuka katika mikutano ya hadhara ya makundi hayo mawili ya wafuasi wa serikali na wale wa upinzani kati kati mwa mji mkuu, Bishkek. Wapinzani wa serikali wamekuwa wakijaribu kuleta mabadiliko ya katiba ili kumlazimisha rais Kurmanbek Bakiyev ajiuzulu. Rais Bakiyev alitupilia mbali madai hayo. Serikali imewatuhumu wapinzani kutaka kuchukuwa madaraka kwa nguvu wakati wameitisha kikao cha dharura cha bunge. Rais Bakiyev ametishia kulivunja bunge ikiwa hakutapatikana suluhu la kisiasa na upinzani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com