BISHKEK : Muafaka wa katiba mpya wafikiwa
8 Novemba 2006Matangazo
Maafisa wa serikali na wale wa upinzani nchini Uzbekistan imeripotiwa kuwa wamefikia makubaliano na Rais Kurmanbek Bakiyev juu ya katiba mpya ambayo inaweza kusaidia kuuzima mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo ambao uligeuka kuwa ghasia hapo jana.
Upinzani umekuwa ukidai katiba mpya ambayo itapunguza sana madaraka ya rais.
Hali hiyo imepelekea kufanyika kwa mfululizo wa maandamano dhidi ya rais ambapo maelfu kwa maelfu ya waandamanaji walimiminika mabarabarani katika mji mkuu wa Bishkek.
Takriban watu 35 wamejeruhiwa katika ghasia hapo jana ambapo polisi ilitumia mabomu ya kutowa machozi.