BETHLEHEM : Viongozi wa kidini wahimiza amani | Habari za Ulimwengu | DW | 25.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BETHLEHEM : Viongozi wa kidini wahimiza amani

Maelfu ya watu wamesheherekea Mkesha wa X’masi katikati ya Bethelehem hapo jana na kujitahidi kuondowa kiwingu cha mashaka kilichogubika mahala alikozaliwa Yesu Kristo.

Misa ya Mkesha wa X’masi ilifanyika kwenye Kanisa la St.Catherine linalopakana na Kanisa la Nativity mahala pa asili alikozaliwa Yesu.

Katika mahubiri yake Askofu Mkuu Michael Sabbah amemuombea baraka Rais Mahmoud Abbas wa Palestina aliyehudhuria misa hiyo na kuwataka Wapalestina kukomesha mapambano yao ya hivi karibuni baina ya makundi pamoja na umwagaji damu kati ya Israel na Wapalestina.

Amesema mzozo huo umedumu kwa muda mrefu na kwamba wakati umefika wa kuanza awamu mpya katika historia ya ardhi hiyo takatifu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com