BERLIN:Wafanyikazi wa Deutsche Telekom kuandamana | Habari za Ulimwengu | DW | 12.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Wafanyikazi wa Deutsche Telekom kuandamana

Takriban wafanyikazi alfu 8 wa kampuni ya simu ya kitaifa ya Deutsche Telekom wanatarajiwa kuandamana ili kupinga mabadiliko katika kampuni hiyo.Kampuni hiyo inapanga kuhamisha wafanyikazi alfu 50 kuhudumu kwenye kampuni nyengine ndogo katika mazingira tofauti ya kazi.

Kulingana na shirika la wafanyikazi la Verdi yapata wafanyikazi alfu 8 wnaatarajiwa kuandamana kote nchini huku viongozi wa kampuni ya Deutsche Telekom na wawakilishi wao wakikutana kwa mara ya tatu kujadilia mipango ya kubana matumizi.

Mazungumzo yanapangwa kufanyika hii leo na kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com