BERLIN:Ujerumani kutafakari jukumu la jeshi lake nchini Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Ujerumani kutafakari jukumu la jeshi lake nchini Afghanistan

Baraza la mawaziri la Ujerumani leo linatafakari jukumu la kulinda amani linalotekelezwa na wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Ujerumani inakusudia kuimarisha kazi za ujenzi mpya kwa kuongeza msaada wa fedha hadi kufikia Euro milioni 125.

Kwengineko waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora anakutana leo hii na kansela Angela Merkel wa Ujeruman mjini Berlin.

Baadae waziri mkuu wa Lebanon atakutana pia na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier na waziri wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-zeul.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com