BELGRADE: Mtuhumiwa uhalifu wa vitani amekamatwa Montenegro
17 Juni 2007Matangazo
Mkuu wa zamani wa polisi wa Kiserb,aliekuwa akisakwa kwa mashtaka ya uhalifu katika jimbo la Kosovo,amekamatwa Montenegro.Ripoti zinasema mshtakiwa huyo na anapelekwa jela ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague,nchini Uholanzi.Vlastimir Djordjevic ameshtakiwa kuhusika na mauaji na mateso ya wakazi wenye asili ya Kialbania,wakati wa vita vya Kosovo,kati ya mwaka 1998 na 1999.Wakati huo,Djordjevic alikuwa Naibu Waziri wa ndani wa Serbia na kamanda wa polisi pia.