Beirut. Solana awataka viongozi wa Lebanon kutatua mgogoro wa uongozi haraka. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Beirut. Solana awataka viongozi wa Lebanon kutatua mgogoro wa uongozi haraka.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana amewataka viongozi wa Lebanon kutafuta suluhisho la haraka la kisiasa katika mvutano wao uliodumu kwa muda wa miezi minne wa kugombea madaraka.

Solana ametoa matamshi hayo wakati wa ziara yake mjini Beirut, ambako amekuwa na mazungumzo na waziri mkuu Fouad Siniora na spika wa bunge Nabih Berri, ambaye anaunga mkono kundi la upinzani linaloongozwa na Hezboullah.

Solana anaelekea sasa mjini Riyadh kwa mazungumzo na maafisa wa Saudi Arabia kabla ya kusafiri kwenda Damascus Syria kwa mkutano wa rais Bashir al- Assad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com