BEIRUT : Hezbollah yakubali mpango wa amani | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT : Hezbollah yakubali mpango wa amani

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah ameukubali mpango wa Umoja wa Waarabu kutatuwa mgogoro wa Lebanon kati ya kundi hilo la wanamgambo wa Kishia na serikali ya nchi hiyo.

Hatua hii inakuja masaa machache baada mamia kwa maelfu ya wafuasi wa upinzani nchini Lebanon kufanya maandamano makubwa ya umma katika mji mkuu wa Beirut kuendelea kuishinikiza serikali inayoipinga Syria kujiuzuku.Wanadamanaji wanadai kwamba serikali hiyo inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi ya Waziri Mkuu Fouad Siniora haiwawakilishi wananchi baada ya kujiuzulu kwa mawaziri sita wanaoiunga mkono Syria hapo mwezi uliopita.

Siniora anaushutumu upinzani kwa kujaribu kuzuwiya mipango ya kuundwa kwa mahkama ya kimataifa kuwashtaki watuhumiwa wa mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri mjini Beirut hapo mwaka 2005 ambapo Syria inalaumiwa kwa kuwa na mkono wake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com