BEIJING:Olmert awasili Beijing kuishawishi China kupinga mpango wa nuklia wa Iran
9 Januari 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert amewasili mjini Bejing China, kuishawishi nchi hiyo ijinasibishe na nchi za Magharibi dhidi ya mpango wa nuklia wa Iran.
China imejitolea kuwa mpatanishi katika mzozo huo mpya wa mpango wa nuklia wa Iran
Olmet pia anatarajiwa kuitumia ziara hiyo ya siku tatu kuimarisha uhusiano wa kibiashara na China.