Bayern Munich wamuwania mlinzi wa pembeni wa Chelsea. | Michezo | DW | 10.07.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern Munich wamuwania mlinzi wa pembeni wa Chelsea.

Madrid na Barcelona kuanza msimu huu kwa michezo ya nyumbani.

Mchezaji mpya wa Real Madrid Real Cristiano Ronaldo kutoka Ureno akipungia mashabiki siku alipojitokeza kuonyeshwa kwa mashabiki.

Mchezaji mpya wa Real Madrid Real Cristiano Ronaldo kutoka Ureno akipungia mashabiki siku alipojitokeza kuonyeshwa kwa mashabiki.

Katika ukurasa wa michezo leo, Real Madrid na Barcelona za Hispania kuanza ligi viwanja vya nyumbani, Bayern Munich ya Ujerumani bado yahitaji beki wa kulia kabla ya msimu wa Bundesliga kuanza na michezo ya kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati , yaingia katika fainali.Klabu za soka za Barcelona, mabingwa wa soka barani Ulaya na Real Madrid zote za Hispania , zitaanza ligi ya msimu huu kwa michezo ya nyumbani. Vigogo hao wa soka barani Ulaya na Hispania wataanza ligi msimu huu wa 2009/10 nyumbani kwa mujibu wa chama cha kandanda nchini humo.

Mabingwa watetezi Barcelona watafungua dimba dhidi ya Sporting Gijon katika uwanja wa Camp Nou siku ya Jumatatu August 31, siku tatu baada ya kupambana na Shakhtar Donetsk katika kombe la bara la Ulaya la Super Cup, mjini Monaco.

Real Madrid wakiwa na kikosi cha kutisha cha Galacticos , watakuwa nyumbani dhidi ya Deportivo Coruna siku ya Jumapili August 30, katika kile kitakachokuwa kuingia uwanjani kwa mara ya kwanza kwa vifaa vipya vya Galactico, Cristiano Ronaldo, Kaka na Karim Benzema katika mchezo rasmi. Wakati huo huo Real Madrid wanatafuta kupata saini ya mchezaji wa kiungo wa Liverpool Xabi Alonzo, amesema mkurugenzi wa michezo wa Real Pardeza Miguel.

Huko mjini Munich, Bayern Munich inatafuta mlinzi wa kulia kabla ya kuanza msimu wa Bundesliga, mwenyekiti wa klabu hiyo Karl-Heinz Rummenigge amewaambia waandishi habari.

Mwenyekiti huyo wa Bayern amesema kuwa wanamhitaji mlinzi wa Chelsea , Jose Bosingwa akimweleza kuwa ni mchezaji mzuri ambapo ni mmoja kati ya wachezaji bora katika bara la Ulaya katika nafasi hiyo.

Ameongeza hata hivyo kuwa , iwapo itawezekana kupata saini yake kuichezea timu hiyo hilo ni suala la Chelsea ambako ana mkataba wa muda mrefu.

Mchezaji nyota wa Japan Shunsuke Nakamura amewakwepa waandishi habari wa nchini humo jana Ijumaa wakati akiondoka kwenda kujiunga na Espanyol kutoka Celtic, akiwa na nia ya kuonyesha tena uwezo wake ikiwa ni msimu wake wa nane katika ligi za Ulaya.

Alikataa kuzungumza na waandishi habari karibu 50 kabla ya kupanda ndege kutoka uwanja wa ndege wa Narita karibu na Tokyo, akitarajia kutoa maelezo yake katika uwanja wa ndege wa Barcelona siku ya Jumatatu, wakati atakapotia saini makubaliano ya kuichezea Espanyol Barcelona kwa muda wa miaka miwili.

Nae kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew amesema nahodha Michael Ballack anabaki kuwa kiongozi wa timu hiyo ya taifa katika kile anachotarajia kuwa mpambano mkali na Urusi kwa ajili ya kuweza kupata tikiti ya moja kwa moja kwa ajili ya fainali za mwakani za kombe la dunia nchini Afrika kusini.

Loew ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa katika mahojiano siku ya Ijumaa kuwa licha ya tofauti zilizokuwapo kati yake na Ballack lakini mchezaji huyo wa kiungo wa Chelsea atabaki kuwa nahodha wa timu hiyo.


Na huko Afrika mashariki , mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika mashariki na kati kwa vilabu yanafikia hatua ya fainali siku ya jumapili. El Merreikh ya Suda imefanikiwa kuingia fainali baada ya kuishinda TP Mazembe kwa mabao 2-1 katika nusu fainali ya kwanza. Nusu fainali ya

Mwamuzi wa kimataifa kutoka Tanzania Charles Mbagga ambaye yuko nchini Sudan kwa ajili ya michuano hiyo.

Nae rais wa ligi ya soka ya Ujerumani Dr. Reinhard Rauball, ametoa wito kwa shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA kuchukua hatua dhidi ya madeni makubwa ya vilabu pamoja na fedha zinazotumika kuwanunua wachezaji. Amesema kuwa muda umefika kuiambia UEFA kuwa haiwezi kuendelea kufanyakazi kwa njia hii.

Mwandishi Sekione Kitojo /AFPE, DPAE

Mhariri Othman Miraj.
►◄
 • Tarehe 10.07.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IlCb
 • Tarehe 10.07.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IlCb