Barroso alihutubia Bunge la Ulaya | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Barroso alihutubia Bunge la Ulaya

Hotuba yake hiyo ililenga zaidi kuhusu uchumi wa Umoja wa Ulaya na kutoa mapendekezo kadhaa kuzuia mizozo mingine ya madeni.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso amelihutubia bunge la Ulaya kwa mara ya kwanza mjini Strasbourg, akielezea matarajio yake kuhusu uchumi wa umoja huo.

Mwanasiasa huyo wa Ureno, aliwaambia wajumbe wa Bunge la Ulaya kuwa mataifa 27 wanachama wa umoja huo yamekabiliana vizuri na mzozo wa kiuchumi duniani. Hata hivyo, Barroso ameonya kuwa mataifa wanachama yanatakiwa kuungana ili kuufufua uchumi.

Barroso alipendekeza marekebisho kadhaa ili kuzuia mizozo mingine, ikiwemo hatua madhubuti zaidi za kudhibiti soko la fedha na kuanzisha taasisi ya pamoja ya Ulaya kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu.

 • Tarehe 08.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P6ZE
 • Tarehe 08.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P6ZE