Baraza la vyama vya Kijamii zisizo za kiserikali lazinduliwa nchini Tanzania
10 Septemba 2008Matangazo
Jana mjini Dar Es Salaam umoja wa Afrika umezindua rasmi baraza la vyama vya kijamii ama asasi zisizo za kiserikali ambalo linapigiwa upatu kuimarisha uwezo wa bara hilo. Sekione Kitojo alizungumza na mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania wakili Francis Kiwanga ambapo kwanza alitaka kujua kazi hasa za baraza hili.