Baraza la usalama.
17 Aprili 2008
Marekani na Uingereza zimefafanua hatua za kuleta ufanisi katika majukumu ya kulinda amani barani Afrika. Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, katika baraza la Usalama, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Zalmay Khalilzad amesema,majukumu ya kulinda amani yanayotekelezwa na Umoja wa Mataifa barani Afrika yanapaswa kuwekewa malengo ya kufahamika, kuhusu muda na bajeti.
Mkutano baina ya viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa uliitishwa kujadili njia za kuimarisha ushirikiano katika suala la usalama baina ya pande mbili hizo.
Mwenyekiti wa mkutano huo rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amesema ni muhimu kwa majukumu ya kulinda amani barani Afrika kuongezewa fedha.