1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, laadimisha mwaka mmoja.

26 Machi 2007

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa changamoto kwa baraza la kutetea haki za binadamu la Umoja wa mataifa,kutimiza ahadi ya kulinda haki za binadamu Ulimwenguni. Hatahivyo mabalozi wanatabiri kuwa,baraza hilo,halitatekeleza maazimio yake kutokana na mivutano ya kisiasa na mabalozi wa nchi za Mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/CB54

Katika kikao cha nne kilichoanza mapema mwezi Machi,wanchama wa baraza la kutetea haki za binadamu wanakabiliwa na jukumu la kutizama ripoti ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Sudan. Baraza hilo hadi sasa halijapitisha ikiwa visa vya dhulma huko Dafur ni ukiukaji wa haki za binadamu au la. Hatahivyo tayari Washington imetaja matukio ya Dafur kuwa mauaji ya halaiki.

Kadhalika,baraza hilo lililopo Geneva na lenye wanachama 47,limeshtumu Israel kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika maazimio manane. Tayari wanatayarisha maazimio mengine manne ya kuishtumu zaidi taifa hilo la Kiyahudi.

Lakini baraza hilo limeanza kuonyesha udhaifu wake baada ya Idadi kubwa ya wanachama ambao ni wa nchi za kiislamu na kiarabu kupuuzilia mbali ripoti ya ukiukaji wa haki za binadamu uliotokana na vita kati ya Israel na Hezbollah, kwa madai kuwa ilidhihirirsha ukiukaji wa haki za binadamu kutoka pande zote mbili badala ya kuonyesha upande mmoja tuu wa Israel. Kwa ufupi Israel pekee ndiyo walio na makosa.

Ban Ki Moon,katibu mkuu wa uomjha wa mataifa alisema "Ulimwengu unawatizama ikiwa baraza hili lililo changa mno,litatekeleza ahadi zake’’. Na kufikia June ambapo baraza hilo litasherekea mwaka mmoja tangu lilipoanza kazi,Ban anatarajia litaweza kutizama na kurekebisha rekodi ya mataifa mbalimbali kuhusu haki za binadamu bila mapendeleo.

Wiki iliyopita,Marekani iliamua kutochukua nafasi ya uwakilishi katika baraza hilo,hatua iliyoonekana kama upinzani wa kidipolmasia dhidi ya baraza hilo la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Lakini licha ya malumbano hayo,Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon alidokezea baraza hilo,liwajibike kudhihirisha kwamba,linaweza kutekeleza majukumu yake bila ushawishi wowote.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu Human Rights Watch na Amnesty International yameshtumu hatua ya Marekani kukataa kuchukua nafasi ya uwakilishi kama walivyofanya mabalozi wengine wa Geneva.

Balozi wa Mexico,Luis Al de Alba Alisema ‘’ni maskitiko makubwa kwa baraza hili kukosa mwakilishi mwenye ushawishi mkubwa duniani kama Marekani’’

Mkurugenzi wa UN Watch, Hillel Neuer, Marekani ingepambana na baraza hilo kwa kuwepo katika nafasi yake kuliko kulishtumu wakiwa nje. Wachanguzi wa kisiasa wanasema tangu baraza hilo kudhihirisha maonevu dhidi ya Israel,kutokubali ripoti ya Dafur,Korea kaskazini, Cuba na Burma,kwao limekuwa kama hakuna maana.

Baraza kuu la Umoja wa mataifa liliunda baraza hilo mwezi Machi mwaka jana kuchukua nafasi ya tume iliyokuwepo ya kuetetea haki za binadamu. Tume hiyo lilikumbwa na kashfa za kuteua wanachama kama Libya,ambao tangu jadi walishindwa kulinda haki za raia wao.

Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa koffi Annan,Novemba mwaka 2006 alishtumu baraza hilo kwa kutilia mkazo juu ya Israel huku ikisahau majukumu yake kwa nchi zilizo na matatizo zaidi kama Sudan. Ni dhahiri baraza hili litakuwa na wakati mgumu wa kuthibithisha uadilifu wake.

Isabella Mwagodi