1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la kitaifa latangazwa nchini Guinea.

Abdu Said Mtullya24 Desemba 2008

Wanajeshi waliotwaa serikali nchini Guinea wametangaza baraza la kitaifa.

https://p.dw.com/p/GMJp
Guinea na nchi inayopakana nazo.Picha: AP / DW

CONAKRY.

Wanajeshi waliotwaa  serikali nchini Guinea  wametangaza baraza  la kitaifa lenye  wajumbe 32.

Baraza hilo la mpito ndilo  litakaloongoza nchi.  Wanajeshi  hao      wameiangusha serikali muda mfupi baada ya kifo cha rais Lansana Conte.

Mkuu wa baraza hilo atakuwa kiongozi wa  wanajeshi waliotwaa serikali, kapteni Mussa Dadis Camara.Raia sita pia wameteuliwa  kuwamo  katika  baraza hilo.

Hatahivyo  spika wa bunge  Aboubacar Sompare  amesema    anaamini kuwa wanajeshi  waliojaribu  kutwaa serikali ni watu wachache na kwamba  hawaungwi mkono jeshini.

Wakati  huo huo  ,Baraza  la amani  na usalama la  Umoja  wa  Afrika linakutanakujadili hali  ya  nchini Guinea kufuatia hatua  ya  kundi la wanajeshi kujaribu kuianhusha serikali.