Ban Ki-moon kwenda Pakistan kuwaona wahanga wa mafuriko | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Ban Ki-moon kwenda Pakistan kuwaona wahanga wa mafuriko

Mtu wa kwanza anayeugua ugonjwa wa kipindupindu ameripotiwa nchini Pakistan kufuatia mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini katika miaka kadha.

Walionusurika na mafuriko nchini Pakistani wakipambana kupata mahitaji yanayotolewa na jeshi la nchi hiyo.

Walionusurika na mafuriko nchini Pakistani wakipambana kupata mahitaji yanayotolewa na jeshi la nchi hiyo.

Islamabad.

Mtu wa kwanza anayeugua ugonjwa wa kipindupindu ameripotiwa nchini Pakistan kufuatia mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini humo katika miaka kadha. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon , ambaye anatarajiwa kuwasili nchini Pakistan mwishoni mwa juma hili, ameonya kutokea wimbi la pili la vifo kutokana na magonjwa. Ban anatarajiwa kukutana na wahanga pamoja na mashirika ya kutoa misaada. Mkuu wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu Pascal Cuttat amesema.

Mkuu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake John Holmes ametoa wito wa kupatiwa kiasi cha dola milioni 460 za msaada wa dharura. Zaidi ya dola milioni 100 zinahitajika kwa ajili ya kuwahifadhi mamilioni ya watu ambao hawana makaazi. Pakistan na Umoja wa Mataifa zinakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 13 wameathirika na maafa hayo ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,600.

 • Tarehe 14.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OngF
 • Tarehe 14.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OngF
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com