BAGHDAD:Umwagikaji wa damu waendelea Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 07.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Umwagikaji wa damu waendelea Iraq

Washambuliaji wa kujitoa muhanga walijiripua ndani ya gari na kuua watu 20 na kujeruhi wengine zaidi ya 40 karibu na mji wa Ramadi hii leo.Hapo jana takriban watu 33 waliuwawa na 80 kujeruhiwa kwenye shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari karibu na soko lenye watu wengi katika eneo linalokaliwa na washia la Bayya mjini Baghdad.

Katika opresheni yao ya kuweka usalama mjini humo wanajeshi wa Marekani wamewauwa wanamgambo 10 katika mji wa Sadr na kuharibu mahala panapodaiwa kutumiwa na wanamgambo kuwatesa watu.

Kaskazini mwa Baghdad kwenye eneo la Sammara washambuliaji wawili wakujitoa muhanga walivamia vituo vya polisi na kujiripua ndani ya gari na kuua watu kiasi cha maafisa wa polisi 12 na kujeruhi wengine wengi.

Wakati huo huo jeshi la Marekani limesema wanajeshi wake tisa waliuwawa hapo jana sita kati yao waliuwawa katika shambulio la bomu lililotokea kwenye eneo la Diyala.Mwanahabari mmoja pia aliuwawa katika shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com