BAGHDAD: Watu wanne wauwawa katika shambulio la jeshi la Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu wanne wauwawa katika shambulio la jeshi la Marekani

Watu wanne wameuwawa na wengine 25 kujeruhiwa wakati wanajeshi wa Marekani na wa Irak walipowashambulia wanamgambo wa kishia katika mji wa Diwaniyah nchini Irak.

Harakati ya kuwasaka wapiganaji wa kishia mjini humo iitwayo ´Operation Black Eagle´ ilianza jana huku mapambano makali baina ya wanajeshi na wapiganaji yakiendelea kuchacha.

Duru za hospitali zinasema majeruhi 25 wamelazwa katika hospitali ya mjini Diwaniya lakini kuna hofu kwamba magari ya kubebea wagonjwa hayawezi kuwafikia majeruhi wengine katika uwanja wa mapambano.

Jeshi la Marekani limesema lilifanya shambulio la angani baada ya kupata taarifa kutoka kwa wakaazi wa mjini humo. Lengo la harakati hiyo ni kuvuruga juhudi za waasi mjini humo na kurejesha udhibiti wa mji huo kwa serikali.

Sambamba na taarifa hiyo, serikali ya Irak imekubali kufanya mkutano utakaozijumulisha nchi jirani na dola kuu duniani utakaofanyika nchini Misri mwezi uliopita.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Misri, Ahmed Gheit amethibitisha kuwa mkutano huo utafanyika mahali pa mapumziko huko Sharm el Sheikh katika bahari nyekundu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com