1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wapiganaji wa Irak wabadili mbinu za mashambulizi

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPQ

Maafisa wa jeshi la Marekani nchini Irak wamesema waasi wa Irak wanatumia mbinu mpya kufanya mashambulizi. Wapiganaji hao sasa wanatumia gesi za sumu.

Mkurugenzi wa hospitali moja mjini Baghdad amesema madaktari wamekuwa wakiwatibu wagonjwa kadhaa walioathirika na sumu ya gesi ya chlorine baada ya wanamgambo kuyashambulia maeneo ya raia na kuripua kwa mabomu magari ya kubeba gesi hiyo.

Mashambulizi hayo ya mabomu yaliyofanywa mjini Baghdad na katika mji jirani wa Taji yamewaua watu wanane na kuwajerhi wengine wengi kutokana na gesi hiyo ya sumu.

Msemaji wa jeshi la Marekani mjini Baghdad, meja jenerali William Candwell amesema mbinu za wapiganaji wa Irak zimebadilika lakini mkakati bado haujabadilika.

´Tunachokiona ni kwamba mbinu zimebadilika lakini mkakati ni ule ule wa kufanya mashambulio ya hali ya juu kuwatisha Wairaki. Katika miezi michache iliyopita juhudi zimefanywa kuongeza kiwango cha ugaidi kwa kuchanganya kemikali za kawaida na vifaa vya kulipuka kujaribu kutia hofu miongoni mwa Wairaki.´

Wakati huo huo, wanajeshi wa Marekani na wa najeshi wa Irak wamekuwa katika haliy a tahadhari katika kumbukumbuku ya mwaka wa kwanza tangu shambuliodhidi ya msikiti wa Al Askari mjini Samara.

Shambulio hilo dhidi ya mojawapo ya sehemu takatifu za waislamu wa madhehebu ya Shia lilichochea wimbi la umwagaji damu wa kimadhehebu ambalo linaisukuma Irak kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.