BAGHDAD: Wanne wauwawa katika shambulio la kujitoa muhanga | Habari za Ulimwengu | DW | 25.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanne wauwawa katika shambulio la kujitoa muhanga

Takriban watu wanne wameuwawa katika shambulio la kujitoa muhanga kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Baghdad nchini Irak.

Watu wengine 14 wamejeruhiwa katika shambulio hilo wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipoingia na kujilipua ndani ya kituo cha polisi cha mji wa Balad Ruz katika jimbo la Diyala.

Wanajeshi tisa wa Marekani waliuwawa katika mkoa huo wa Diyala siku ya jumatatu.

Watu wengine 20 walijeruhiwa katika shambnulio hilo baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha mwaka mmoja.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com