Baghdad. Wanajeshi 11 wa Iraq wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Wanajeshi 11 wa Iraq wauwawa.

Duru za jeshi la usalama nchini Iraq zinasema kuwa bomu lililokuwa limewekwa katika lori limelipuka na kuuwa wanajeshi 11 wa Iraq katika mji wa kaskazini wa Al-Sharkat.

Jeshi la Marekani limesema kuwa watoto watatu wameuwawa katika shambulio hilo ambalo linasadikiwa limefanywa na wapiganaji katika jimbo lenye machafuko la Anbar.

Wanajeshi waliokuwa katika kifaru cha jeshi la Marekani waliwafyatulia risasi watu watatu ambao wanaaminika kuwa walikuwa wanatega bomu katika barabara kuu kusini mashariki ya mji wa Fallujah, kilometa 65 magharibi ya Baghdad.

Jeshi limesema kuwa haijafahamika iwapo watoto hao wamekufa kutokana na shambulio hilo ama mlipuko wa pili kutokana na bomu lililokuwapo katika eneo hilo, lakini tukio hilo linachunguzwa.

Kwingineko nchini Iraq, mwanajeshi wa Marekani ameuwawa kwa kupigwa risasi katikati ya mji wa Baghdad.

Mjini Baquba , mtu aliyejitoa muhanga alijilipua katika jengo ambalo linawahifadhi wapiganaji walioamua kuachana na mapambano, na kusababisha vifo vya watu wawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com