1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Walinzi wa kigeni walaumiwa kwa kuuwa

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H0

Serikali ya Iraq inalaumu walinzi wa usalama wa kigeni kwa kupigwa risasi na kuuwawa kwa wanawake wawili wa Iraq katikati ya Baghadad hapo jana.

Maafisa wanasema walinzi hao wa kampuni yenye makao yake mjini Dubai walilifyetulia risasi gari waliokuwemo wanawake hao wakati lilipokuwa likiwakaribia.

Mauaji hayo yamekuja siku ambapo serikali ya Iraq imetaka kampuni ya Kimarekani ya Blackwater kulipa jumla ya dola milioni 136 kwa familia za watu 17 waliouwawa na walinzi wa kampuni hiyo mwezi uliopita.