BAGHDAD: Umwagaji wa damu waendelea Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 22.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Umwagaji wa damu waendelea Irak

Afisa wa Kiiraki ameuawa baada ya kutekwa nyara kaskazini-mashariki ya mji mkuu Baghdad.Msemaji wa polisi amesema,afisa huyo wa polisi,Brigedia Falah Khalaf,alitekwa nyara asubuhi ya leo alipokuwa njiani kwenda kazini kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani.Muda mfupi baadae,maiti ya afisa huyo iligunduliwa ndani ya gari lake.

Wakati huo huo,bomu lililoripuka kando ya barabara,katika wilaya ya Amin,kusini mashariki ya Baghdad,limemuua raia mmoja na kuwajeruhi wengine watano.Bomu hilo liliripuka,basi la usafiri wa umma lilipokuwa likipita barabarani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com