Baghdad. Shambulio la bomu laua watu 115. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Shambulio la bomu laua watu 115.

Kijiji kimoja upande wa kaskazini mwa Iraq kimeshambuliwa kwa bomu la kujitoa muhanga ambalo limesababisha kiasi cha watu 115 kuuwawa.

Magari ya kubeba wagonjwa yalifika haraka katika eneo la soko lililokuwa na watu wengi katika mji ambao unakaliwa na watu wengi wa madhehebu ya Shia wa Tuz Khurmatu ambako mlipuko huo umetokea.

Mkuu wa polisi amesema kuwa idadi ya watu waliofariki inaweza kupanda zaidi baada ya bomu hilo kuvunja maduka na nyumba ndogo ndogo.

Waziri mkuu Nuri al- Maliki amesema kuwa kitendo hicho cha kikatili kinathibitisha kuwa magaidi ni maadui wa Wairaq wote. Shambulio hilo lilikuwa ni baya zaidi tangu Aprili 18 mwaka huu, wakati watu 190 walipouwawa katika wimbi la mabomu dhidi ya wilaya inayoishi Washia katika mji wa Baghdad.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com