BAGHDAD: Mmuagiko wa damu unaendelea nchini Irak
12 Novemba 2006Matangazo
Mashambulio ya bomu leo hii yamesababisha tena mmuagiko mkubwa wa damu nchini Irak.Katika shambulio moja la kujitolea muhanga lililofanywa magharibi mwa mji mkuu Baghdad,kwenye kituo cha polisi cha kuandikisha kazi,watu 34 waliuawa na si chini ya 60 wamejeruhiwa.Shambulio jingine la bomu lililotegwa kando ya barabara na kuwalenga polisi waliokuwa wakipiga doria mashariki mwa Baghdad,liliwaua wapita njia wanne wa Kiiraki na mmoja alijeruhiwa.