1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maafisa 10 wa usalama wauwawa

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBf2

Wapiganaji nchini Irak wamewaua maafisa 10 wa usalama hii leo huku wanajeshi wanaongozwa na Marekani wakifanya uvamizi unaolenga kukomesha upinzani nchini humo.

Katika shambulio la kwanza maafisa watano wa polisi waliuwawa wakiwa katika doria baada ya bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara kulipuka wakati gari lao lilipokuwa likipita eneo la al Dagharah yapata kilomita 120 kusini mwa mji mkuu Baghdad. Maafisa wengine wawili wamejeruhiwa kwenye hujuma hiyo.

Maafisa wengine watano wa usalama wakiwemo wanajeshi watatu wa Irak na maafisa wawili wa polisi wameuwawa wakati walipofanya uvamizi wa pamoja dhidi ya ngome ya al-Qaeda katika mji wa Tikrit kaskazini mwa Irak.

Sambamba na hayo watu sita wameuwawa na wengine 13 kujeruhiwa wakati mtu wa kujitoa mhanga maisha alipojilipua kwenye lango la kuingilia kituo cha polisi katika eneo la Tal Abta kaskazini mwa Irak.