BAGHDAD : Iraq yafanya mkutano wa usuluhishi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Iraq yafanya mkutano wa usuluhishi

Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki amesema kwamba jeshi la taifa limefunguwa milango kwa wanajeshi wa zamani wa Saddam Hussein ambao walipoteza nyadhifa zao kufuatia uvamizi uliongozwa na Marekani nchini humo.

Maliki pia amesema yuko tayari kuzungumzia suala la amani ya nchi hiyo na wanachama wa zamani wa chama kilichopigwa marufuku cha Baath cha Saddam ambao hawakuhusika na uhalifu dhidi ya wananchi wa Iraq.

Kauli yake hiyo inakuja wakati serikali ya Iraq ikiwa imeitisha mkutano wa usuluhishi wa kitaifa wenye lengo la kukomesha mapigano ya madhehebu nchini Iraq.

Wanasiasa kutoka vyama vya Washia,Wasunni na Wakurdi ni washiriki wakuu wa mkutano huo ambao unasusiwa na waasi wa Kisunni wa msimamo mkali pamoja na Washia wa itikadi kali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com