Baba wa muziki soul James Brown afariki | Habari za Ulimwengu | DW | 25.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baba wa muziki soul James Brown afariki

Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa soul James Brown amefariki leo alfajiri huko Atlanta Georgia akiwa na umri wa miaka 73.

James Brown alipelekwa hospitali wiki hii alikolazwa kutokana na maradhi ya Nimonia, kabla kufariki leo asubuhi.

James Brown ambaye alizaliwa mwaka 1933, aalikuwa akijulikana kama baba wa muziki wa soul ambapo katika miaka 60 na 70 aliubadilisha muziki wa soul na kujipatia umaarufu mkubwa.

Wengi wanamchukulia James Brown kama ndiyo chachu ya mafanikio ya wanamuziki wengi wa muziki wa soul kama vile Micheal Jackson.

Mnamo mwaka 1968 James Brown alilazimika kupiga muziki katika kituo cha radio huko Boston usiku kucha katika kupunguza hasira za watu na fujo kufuatia mauaji ya mwanaharakati mwmeusi Martin Luther King Jr

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com