ABUJA: Wafanyakazi wa kampuni la mafuta watekwa nyara | Habari za Ulimwengu | DW | 25.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: Wafanyakazi wa kampuni la mafuta watekwa nyara

Si chini ya wafanyakazi 6 wa kampuni la mafuta wametekwa nyara kusini mwa Nigeria.Watu wenye bunduki walishambulia mashua ya wafanyakazi waliokuwa wakiweka mabomba ya mafuta,nje ya pwani ya jimbo la Bayelsa lililokuwa na utajiri mkubwa wa mafuta.Mara kwa mara,wafanyakazi wa makampuni ya mafuta hutekwa nyara katika eneo hilo la Niger Delta,na wanamgambo wanaotaka kuwa na usemi zaidi kuhusika na utajiri wa mafuta katika eneo lao.Kwa kawaida,baada ya malipo ya pesa,mateka huachiliwa huru bila ya kuumizwa.Zaidi ya wageni na Wanigeria 100 wametekwa mwaka huu.Nigeria ni mzalishaji mkubwa kabisa wa mafuta barani Afrika. Asilimia 90 ya pato lake la mwaka hutokana na bidhaa hiyo ya mafuta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com