1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Utawala wa kijeshi waandaa maandamano

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7G8

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umekataa mwito wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kuanzisha mazungumzo na upande wa upinzani unaotetea demokrasia.

Utawala wa kijeshi umesema umesikitishwa na taarifa ya baraza la usalama la umoja wa mataifa iliyokosoa hatua ya kutumiwa nguvu dhidi ya waandamanaji hivi karibuni.

Serikali ya mjini Yangoon imesema kwamba mwito wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa pamoja na waandamnaji wanaozuiliwa hauafiki matakwa ya umma wa Myanmar.

Wakati huo huo utawala wa kijeshi umeandaa maandamano makubwa mjini Yangoon.

Waanadamanji wanaoiunga mkono serikali ya kijeshi walikusanyika kwenye uwanja wa michezo mapema leo kushiriki mkwenye maandamano hayo.