1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Maandamano

Maandamano ni hatua inayochukuliwa na kundi au makundi ya watu wanaopigania jambo la kisiasa au vinginevyo; kwa kawaida yanahusisha matembezi ya watu wengi na ama kuanza na au kukutana mahala pa mwisho palipoainishwa.

Vitendo kama vile vizuwizi na ukaliaji wa maeneo vinaweza pia kuchukuliwa kama maandamano. Maandamano yanaweza kuwa ya vurugu au yasiyo ya vurugu. Au yanaweza kuanza ya amani na kuishia kuwa ya vurugu kutegemea na mazingira. Wakati mwingine polisi wa kuzuwia ghasia au idara nyingine za sheria huingilia kati. Baadhi ya wakati hii inaweza kuwa na lengo na kuzuwia maandamano hayo yasifanyike, au kuzuwia vurugu kati ya makundi hasimu. Katika ukurasa huu utakuta maudhui za DW kuhusu maandamano.

Onesha makala zaidi