Wolfowitz kuongoza jopo la ushauri kwa serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wolfowitz kuongoza jopo la ushauri kwa serikali

Rais wa zamani wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz, ameteuliwa kuongoza jopo la ushauri kwa serikali ya Marekani.

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ilitangaza uteuzi wa bwana Wolfowitz kuwa mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa usalama wa kimataifa inayoongozwa na waziri wa mashauri ya kigeni Condoleezza Rice.

Bodi hiyo ina kibarua cha kutoa uchambuzi na mapendekezo kuhusu maswala yaliyo na umuhimu mkubwa kwa waziri wa mambo ya kigeni mara kwa mara.

Paul Wolfowitz, ambaye anasifiwa kwa kulisaidia bara la Afrika wakati alipokuwa kiongozi wa benki ya dunia, alilazimika kuacha kazi mnamo tarehe 30 mwezi Juni mwaka jana baada ya kukabiliwa na kashfa ya kumpandisha cheo mpenzi wake Shaha Rizza kinyume cha sheria za benki hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com