1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ujerumani aonya kuhusu ushawishi wa Urusi Afrika

Zainab Aziz
4 Machi 2024

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani, Svenja Schulze, amesema magaidi na malengo ya Urusi yanatishia usalama wa eneo la Sahel kusini mwa jangwa la Sahara.

https://p.dw.com/p/4d8PP
Ujerumani Berlin | Waziri wa ushirikiano wa Maendeleo Schulze
Waziri Schulze anaelekea Burkina Faso na BeninPicha: Ute Grabowsky/photothek/IMAGO

Waziri Schulze amesema hayo kabla ya kuanza ziara nchini Burkina Faso na Benin. Schulze atakuwa waziri wa kwanza wa Ulaya kufanya ziara nchini Burkina Faso tangu wanajeshi watwae madaraka mwaka mnamo 2022.

Waziri huyo ni mwenyekiti wa Muungano wa Sahel, ulioanzishwa na Ujerumani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya ili kuyasaidia mataifa ya Sahel. Ujerumani inashika nafasi ya nne kwa ukubwa wa misaada inayotoa kwa ajili ya nchi za eneo la Sahel.

Burkina Faso, imekuwa inashambuliwa kwa miaka mingi na makundi ya magaidi yanayozidi kuusogelea mji mkuu Ouagadougou. Maalfu kadhaa ya watu waliuawa mwaka jana pekee.Wengine wapatao milioni 2 wamegekuwa kuwa wakimbizi wa ndani.