Waziri mkuu wa Irak aahidi usalama utadhibitiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waziri mkuu wa Irak aahidi usalama utadhibitiwa

Baghdad:

Serikali ya Iraq imeiahidi Marekani kufanya kila liwezekanalo kudhibiti haraka hali ya usalama nchini humo.“Matatizo yanabidi yatatuliwe kwa „kipindi maalum“ wamesema hayo waziri mkuu Nuri al Maliki na balozi wa Marekani mjini Baghdad,Zalmay Khalilzad katika taarifa yao ya pamoja.Taarifa huiyo inashadidia ushirikiano wa dhati ulioko kati ya mataifa hayo mawili.Marekani imeahidi kuendelea kuisaidia serikali ya Irak katika juhudi zake za kuimarisha Demokrasia na utulivu-taariofa hiyo imesema.Wakati huo huo mwanamaji mmoja wa kimarekani amefariki dunia kutokana na majaraha aliyoyapata katika mashambulio dhidi ya waasi huko Al Anbar.Jumla wa wanajeshi 98 wameuwawa tangu mapema mwezi huu nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com